
Wenyeji wa kombe la Copa America Chile wamefuzu kufika fainali mara ya
kwanza kwa miaka 28. Hii ni baada ya kuwanyuka Peru mabao mawili kwa
moja katika mchuano uliofanyika mjini Santiago.
Nusura kiungo wa
kati wa Chile Arturo Vidal kuondolewa mapema, hata hivyo bahati mbaya
ilikua wa mlinda lango wa Peru Carlos Zambrano aliyepewa kadi nyekundu.Aliyekua mshambuliaji wa klabu wa QPR ya Uingereza Eduardo Vargas alisaidia Chile kupata bao la kwanza dakika ya 42.

Chile haijawahi kushinda kombe la Copa kwa karibu karne moja. Chile wanaingia fainali hapo Jumamosi ambapo huenda wakachuana na Argentina au Paraguay.