Marekani wanacheza fainali ya nne ya
Kombe la Dunia kwa wanawake baada ya kuwafunga mabingwa mara mbili wa
kombe hilo, Ujerumani katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Olmpic
mjini Montreal.
Mshambuliaji wa Ujerumani Celia Sasic alikosa
penalti katika dakika ya 58, lakini nahodha wa Marekani Carli Lloyd
alifunga kwa njia ya kichwa dakika kumi baadaye.Zikiwa zimebakia dakika sita mchezo kumalizika, Kelley O'Hara ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba aliifungia timu yake bao lililowahakikishia Marekani kucheza fainali baada ya kufunga akiwa karibu na lango la Ujerumani.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali Japan itapepetana na England Alhamis wiki hii. Na mshindi katika mechi hiyo atavaana na Marekani katika fainali itakayopigwa siku ya tarehe 6 Julai jijini Vancouver.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni