Mwanariadha
wa mbio fupi Justin Gatlin ameweka muda bora zaidi katika mbio za mita
200 na kuwa wa tano duniani aliposhinda mbio hizo nchini Marekani.
Raia
huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 33 ambaye amehudumia marufuku
mbili za utumiaji wa dawa za kusisimua misuli aliweka rekodi ya mda wa
sekunde 19.57 mjini Oregon.Rekodi hiyo imeifuta ile ya sekunde 19.68 aliyoiweka mnamo mwezi May wakati huo ikiwa rekodi bora duniani.
''Nilitaka kutoka ili niweke historia,na hivyo ndivyo nilivyofanya'',alisema Gatlin.
Gatlin ndiye mwanariadha wa mbio fupi aliyetawala mwaka 2015 baada ya kuweka rekodi bora mwaka huu ya sekunde 9.74 katika mbio za mita 100

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni