
PICHA MBALIMBALI ZA TEGETE UWANJANI NDONDO CUP

MAKOCHA YANGA NA GORI MAHIA WAZUNGUMZIA MCHEZO WA KESHO KOMBE LA KAGAME HAPATOSHI UWANJA WA TAIFA JIJINI DARE ESALAAM
KOCHA MKUU WA YA YANGA NA GORI MAHIA PICHANI

Makocha wa timu za Yanga na Gor
Mahia ya Kenya wamezungumzia mchezo wao wa kesho ambao ndio utakuwa
mchezo wa ufunguzi kwenye michuano ya Kagame Cup mchezo utakaopigwa
kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 10:00
za jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Kila kocha ametamba kuibulka na
ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa ni mkali kutokana na ubora
wa vikosi vya timu zao. Yanga ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara
ambayo ilimalizika mwezi Mei mwaka huu wakati wapinzani wao wakiwa
wanaongoza ligi ya Kenya inayoendelea kutimua vumbi nchini humo.

“Nimekuwa Afrika tangu mwaka 1996
hivyo ninauzoefu na soka la timu za hapa kwa muda mrefu, tumefanya
maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuikabili kila timu kwenye michuano
hii. Kitu kikubwa ni kwamba, mimi huwa sidharau mpinzani wangu kwasababu
kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna mtu anayejua matokeo”,
amesema Pluijm.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Gor
Mahia Mcotish Frank Nuttal amesema yeye hana uzoefu mkubwa kwenye soka
la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake (Van Pluijm) lakini
akasisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili Yanga kesho kwenye
uwanja wa Taifa.
“Yanga ni timu kubwa japo
sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu yenye ushindani na mechi
ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo tutajua matokeo”,
amesema kocha huyo.


Kocha mpya wa Real Madrid, Rafa
Benitez jana katika mkutano na waandishi wa habari nchini Australia
ameulizwa hatima ya beki wake, Sergio Ramos.
Ramos, 29, amekuwa gumzo majira
haya ya kiangazi na inaelezwa kwamba Mhispania huyo anataka kuondoka
Real kutokana na kukosekana kwa maelewano baina yake na uongozi wa
klabu.
Manchester United wamekuwa
wakihusishwa kumsajili Ramos, wakati huo huo nao Real Madrid wakiomba
kumsajili golikipa wa Old Trafford, David De Gea.
Je, Benitez amaejibu nini?
Kocha huyo wa zamani wa
Liverpool na Chelsea amethibitisha kwamba Man United wanamuwinda Sergio
Ramos, lakini akawaambia watu wengi waliohudhuria mkutano huo kuwa
mlinzi huyo kisiki hauzwi.
‘Kuna mengi yanazungumzwa
kuhusu hatima ya Ramos. Mimi nashangaa kwasababu mchezaji mwenyewe
anajituma kwenye mazoezi na anafanya kila kitu timu inataka na mimi pia
ninachotaka”.
Tayari Rais amezungumzia hilo kuwa Ramos atabakia klabuni.
Nimezungumza naye kwa kirefu
kuhusu hatima yake. Naona Segio ni mtu muhimu kwenye timu. Ni mshindi na
ndio maana tunamhitaji kwenye timu”. Amesema Benitez.
Wakati huo, mpenzi wa Ramos,
Pilar Rubio ambaye ni mjamzito amewaambia waandishi wa habari wiki hii
kwamba atakwenda Manchester kama mpenzi wake akiuzwa na akathibitisha
kwamba wameanza kujifunza kuongea kiingereza.
RONALDO AANZA RASMI MAZOEZI KUJIANDAA NA MSIMU MPYA LIGI KUU HISPANIA

Cristiano Ronaldo kiasili ni mtu wa ushindani, anapenda kushinda bila kujali ni tukio gani anashindania.
Mwanasoka huyo anayeshikilia tuzo ya Ballon D’Or
ameshangilia ushindi mdogo tu katika mazoezi na wenzake kama anavyofanya
kwenye mechi za ligi ya mabingwa.
Cheki hapa alivyofanya baada ya kufanikiwa kuingiza mpira na kumfumua Illaramendi Wakati wa mazoezi ya cone drill.
Ameshangilia staili yake ya ‘SIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!’ baada ya kupata pointi kama alivyofanya baada ya kushinda Ballon D’Or mwezi Januari mwaka huu,
Maskini Illara.
c
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni